Karibu wengi wetu tunao msukumo ambao kwa jumla ni wa kisilika wa kutamani mambo yale yatakayotokea baadaye. Tunataka kujua ni kitu gani kilicho mbele ya upeo wa macho yetu. Lakini utabiri uliosahihi huteleza vibaya sana. Tunao wakati mgumu wa kutosha kuweza kujaribu kubashiri hali ya hewa itakayokuwako kesho!
Lakini yuko Mmoja ambaye unabii wake umethibitika kwamba ni sahihi kwa namna ya kustaajabisha sana. Yesu Kristo, kupitia katika Neno lake, anaweza kutuchukua mpaka siku zile za usoni; yeye ni kiongozi anayetegemewa. Katika somo hili tutaangalia kile alichosema yeye juu ya kuja kwake mara ya pili. Kwa vyo vyote vile, ni nani, basi, ambaye angeweza kujua mengi sana juu ya mwisho wa dunia hii zaidi ya yule aliyeiumba pale mwanzo?
