Je! wengi wanaweza kukosea?
Masomo Yote
Sehemu 1 ya 9
SOMO 21Hatua 1 ya 9 (11%)

Je! wengi wanaweza kukosea?

Katika Mwongozo 16 tuligundua kwamba kulionja pumziko la Sabato ni tiba muhimu kwa maisha ya siku hizi yaliyojaa msongo mwingi. Kwa kuwa Mungu anaelewa kila haja tuliyonayo , aliiweka kila siku ya saba kwa ajili ya pumziko letu la kimwili na burudiko letu la kiroho. Baada ya kuiumba dunia yetu kwa siku sita, yeye "akapumzika" katika siku ile ya saba, "akaibariki" na "kuifanya takatifu" (mwanzo 2:1-3).

Mungu alipowapa watu wake Amri kumi, yaani, wana wa Israeli, aliiweka amri ya kuitunza Sabato ya siku ya saba katikati ya sheria yake (Amri kumi) (Kutoka 20:8-11). Kulingana na amri hiyo, Sabato ni ukumbusho wa uweza wa Mungu wa Uumbaji, ni siku ya kutulia na kutafakari juu ya uzuri na maajabu ya kazi zake alizoziumba, ni siku ya kustarehe na kumkaribisha sana Muumbaji wetu, siku ya kuchunguza kwa kina zaidi uhusiano wetu na yeye.

Katika kipindi kile cha maisha ya kibinadamu ya Yesu aliyoishi hapa duniani, yeye pia aliitunza Sabato (Luka 4:16) na kuiidhinisha kama siku inayowaletea Wakristo manufaa (Marko 2:27,28.) Mafungu kadhaa katika kitabu cha Matendo yanaonyesha wazi kwamba wanafunzi wake Kristo waliabudu katika siku ya Sabato baada ya ufufuo wake (Matendo 13:14, 16:13, 17:2, 18: 1-4, 11).

1. Suala Lenye Utata

Hiyo inatufikisha sisi kwenye somo ambalo wengi huliona kuwa lina utata kwao. Kwa kipindi fulani ulimwengu wa Kikristo umekuwa ukizitunza siku mbili tofauti. Kwa upande mmoja, Wakristo wengi sana kwa unyofu wa moyo wanaitunza Jumapili, siku ya kwanza ya juma, ambayo wao wanaamini kwamba ndiyo ukumbusho wa ufufuo wake Kristo. Kwa upande ule mwingine, kundi kubwa la Wakristo, nao vilevile wakiwa ni wanyofu wa moyo, wanaamini kwamba Biblia inaipa heshima siku ya saba peke yake kama ndiyo Sabato na ya kwamba hakuna mahali popote inapothibitisha utakatifu wa Jumapili.

Je! inaleta tofauti yeyote juu ya siku gani tunayoitunza kama Sabato? Sisi kama watu walio wanyoofu wa moyo na wenye ari tunaotaka kuijua kweli, ni lazima tujiulize wenyewe swali hili. "Je! Ni jambo gani ambalo ni maana kwa Yesu? Hivi Yesu anataka mimi nifanye nini?

Katika kufikiria uamuzi wa jambo hilo, mambo kadhaa ya maana hayana budi kuwekwa wazi, je ni nani aliyeibadili Sabato kutoka Jumamosi siku ya saba ya juma, kwenda Jumapili siku ya kwanzia ya juma? Je! Hivi Biblia inatoa idhini kwa badiliko kama hilo?Kama jibu ni ndiyo, Je, Mungu, Kristo, au labda wale mitume ndio waliofanya badiliko hilo?

Tutaendelea mbele kwa kuangalia uwezekano wo wote uliopo