Jehanamu ni nini na iko wapi?
Masomo Yote
Sehemu 1 ya 6
SOMO 23Hatua 1 ya 6 (17%)

Jehanamu ni nini na iko wapi?

Kufyatua risasi kipumbavu kulitokea wakati mwanafunzi mmoja alipoingia katika shule yake na kuwaua wanafunzi wenzake kadhaa. Mwanaume mmoja mwenye chuki, ambaye alikuwa amefukuzwa kazi, aliingia mahali pale alipokuwa akifanya kazi zamani na kumpiga risasi mkuu wake wa kazi. Mama mmoja alisukuma gari lake dogo na kulitumbukiza ziwani likiwa na watoto wake wawili ndani yake na kuwazamisha.

Kwa uchache katika mabara mawili maelfu wamechinjwa katika mauaji ya safisha-safisha ya kikabila. Uhasama wa muda mrefu uliochukua karne nyingi kati ya makundi mawili au zaidi ya makabila hayo ndicho chanzo chake. Wanaume, wanawake, watoto, na hata watoto wachanga wamepigwa risasi, wamekatwa-katwa, wamepigwa, na kubakwa.

Kutoa adhabu ya kifo kwa uhalifu huo wa kishenzi, hata kwa wauaji wale walio wakatili sana, kunashutumiwa na wengi. Makundi yaliyo kinyume na hukumu ya kifo yanapinga kwa makelele mengi, wakiita hukumu hiyo kuwa sio ya kibinadamu ati ni "mfumo wa ibada ya kipagani." Wanauliza hivi, je! wauaji hao hawarekebishiki?

Je! njia sahihi ya kibinadamu ya kuwaua wahalifu waliohukumiwa kuuawa ni ipi? Je! ni kile kiti cha umeme? Wengine wanadhani kudungwa sindano yenye sumu ya kufisha ingekuwa ni njia isiyo na maumivu kabisa. Wengine wanatetea kwamba uhai wa mtu ungekoma kwa upesi zaidi kwa kumnyonga.

Lakini katika majadiliano hayo yote yaliyojaa harara juu ya adhabu ya kifo, upo uchaguzi mmoja ambao hakuna mtu anayeufikiria. Hakuna anayependekeza kwamba wale wauaji wakatili, ambao kwa ukatili

wamekomesha maisha ya mtu mwingine, wapatilizwe kwa kuteswa vibaya sana kimwili mpaka wafe. Kwa mfano, hakuna aliyependekeza kwamba wauaji hao wachomwe moto polepole mpaka wafe.

Lakini, basi Wakristo wengi waaminifu wanadhani kwamba Baba yetu aliye mbinguni atatenda vibaya kuliko hivyo. Wao wanasema, waovu ni lazima wateswe vibaya ili kubatilizwa kwa ajili ya dhambi zao. Tena, zaidi sana ya hayo, wanafikiria kwamba maeneo ya Mungu anayoyatumia kuwaulia wahalifu ni mahali pa mateso yasiyo na mwisho.

Ni kitu gani hasa kinachowapata waovu? Je! maangamizi yao yanapatanaje na upendo na haki ya Mungu? Hebu na tuangalie Biblia itupe jibu.

1. Huzuni Kubwa Ya Mwisho Ya Yesu

Kwa miaka 6,000 Mungu amekuwa akiwasihi sana wanaume na wanawake:

Ezekieli 33:11
"Kama mimi niishivyo, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu...mimi sikufurahii kifo cha mtu mwovu, bali napenda mtu mwovu aachane na mwenendo wake mbaya, apate kuishi"

Msalaba ulidhihirisha ni kwa kiwango gani Mungu anataka kuwaokoa wanadamu walioanguka [dhambini]. Yesu alipopaza sauti pale msalabani, akisema, "Baba uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo," aliufunua wazi moyo wake uliokuwa ukimwuma (Luka 23:34). Muda mfupi baada ya hapo Yesu akakata roho, na kama wengine waaminivyo, akafa kwa kupasuka moyo wake (Yohana 19:30,34).

Lakini hata pamoja na udhihirisho huo wenye nguvu ya upendo wa Mungu, watu wengi bado hawamgeukii Yesu. Na kadiri dhambi inavyoendelea kutawala katika dunia hii, ndivyo itakavyozidi kuongeza misiba ya wanadamu. Kwa hiyo ni lazima dhambi iteketezwe kabisa. Je! hivi Mungu anapanga kufanya nini ili kuikomesha hiyo dhambi?

2 Petro 3:10
"Siku ya Bwana itakuja…. mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu; na vitu vyake vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo dunia itatoweka..."

Hatimaye ni lazima Mungu aitakase dunia hii kutokana na uovu wake na kuikomesha dhambi kabisa. Wale wanaoendelea kung'ang'ania dhambi hatimaye watateketezwa kwa moto huo ulioandaliwa kwa ajili ya kumteketeza Iblisi, malaika zake, na dhambi katika dunia yetu hii. Ni wakati wa kuhuzunisha jinsi gani kwa Yesu anapouangalia moto ukiwateketeza wale aliokuja kuwafia ili kuwaokoa.