Sehemu ya 1
Kristo Alikuwako Tangu Milele
Yesu hakuwa tu mtu mwema, alikuwa Mungu pia. Je, ni madai gani aliyoyatoa Yesu mwenyewe kuhusu Uungu wake?
Yohana 14: 7-9
“"Kama mngalinijua mimi kweli kweli, mngalimjua na Baba. Tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.... Ye yote aliyeniona mimi amemwona Baba"”
Ukitaka kujua jibu kwa maswali haya, "Mungu ni nani? Anafananaje?" unapaswa kumtazama tu Yesu, aliyetangaza, akasema,
Yohana 10:30
“Mimi na Baba Tu umoja”
Mungu Baba na Yesu mwanawe wamekuokoa pamoja tangu milele (Waebrania 1:8.) Haukuwako wakati wo wote ule ambapo Kristo hakuwa umoja na baba yake. Baba yake anatoa upendo na ulinzi wake ule ule kwa kila mtu kama aliouonyesha Yesu katika kipindi cha maisha yake ya kibinadamu hapo duniani.
