mtu akifa, kuna nini baadaye?
Masomo Yote
Sehemu 1 ya 8
SOMO 24Hatua 1 ya 8 (13%)

mtu akifa, kuna nini baadaye?

Tunajikunyata mtoto mdogo anapouliza kwanza swali hili, "kufa maana yake nini? Tunaywea kuzungumza au hata kufikiri juu ya mtu fulani tumpendaye anapokaribia kufa. Mauti ni adui wa watu wote kila mahali. Je! majibu ni yapi kwa maswali magumu yahusuyo kifo? Je! kuna maisha baada ya kufa? Je! tutawaona tena wapendwa wetu waliokufa?

Sehemu ya 1

Kukikabili Kifo Bila Hofu

Sisi sote kwa wakati fulani, labda baada ya kufa rafiki yetu au mpendwa wetu, tumejisikia kana kwamba tumbo liko tupu, yaani, kuwa na hisia ile ya upweke inayopita ndani yetu tunapoangalia kwa haraka kuona mwisho wa uhai wa mtu.

Katika jambo hili la maana sana, lililojaa hisia nyingi, ni wapi basi, tunakoweza kujifunza habari za kile kinachotokea tunapokufa? Kwa bahati nzuri, sehemu ya utume wa Kristo hapa duniani ilikuwa ni "kuwaweka huru wale ambao katika maisha yao yote walikuwa katika hali ya utumwa kwa hofu ya mauti" (Waebrania 2:15). Na katika Biblia, Yesu anatoa ujumbe wenye faraja, kisha anajibu maswali yetu yote juu ya mauti na yale maisha ya baadaye kwa njia inayoeleweka wazi.