Baada ya kuishi karibu maisha yake yote kama mfuasi wa Budha, mtu wa makamo mmoja katika nchi ya Singapore aliyekuwa amegeuka na kuwa Mkristo aliulizwa swali hili, "Bwana Limu, je, wewe unaona tofauti gani kati ya kuwa mfuasi wa Budha na kuwa Mkristo?
"Hilo ni rahisi," alijibu. "Tangu mimi nimempokea Yesu kama Mwokozi wangu, nina amani nyingi ajabu moyoni mwangu."
Hilo ndilo linalotokea tunapoyaweka maisha yetu ndani ya Kristo.
Isaya 26:3
“"Wewe [Mungu] utamlinda katika amani kamilifu, yeye ambaye moyo wake umekutegemea, kwa kuwa anakutumaini"”
Kuishi maisha ya Kikristo huleta amani kamilifu - hisia kamili ya kuwa na usalama na raha.
Wale walioligundua hili wameiona njia pekee ya kupata nafasi ya pili ya kuishi - yaani, kumpata Yesu!
