Siri ya mtindo wa maisha uletao afya
Masomo Yote
Sehemu 1 ya 9
SOMO 18Hatua 1 ya 9 (11%)

Siri ya mtindo wa maisha uletao afya

Watafiti wanaoishi katika kipindi hiki tulicho nacho wamejitahidi sana kuithibitisha ile kweli iliyothibitishwa kwanza na Biblia kwa kutoa maelezo haya: Wanadamu ni viumbe kamili. Mara nyingi kile tunachokigawa katika sehemu za kimwili, kiakili, na kiroho ni sehemu za mtu zilizo na uwiano unaoingiliana, wala hazitenganishiki. Kwa maneno mengine, kinachoidhuru akili, kinaudhuru mwili.Hali yetu ya kiroho ina shinikizo lake juu ya hali yetu ya kimwili, na kinyume chake. Sisi ni watu kamili.

Kwa mfano watafiti wa kisayansi katika uchunguzi wao uliodhibitiwa wamegundua kwamba kicheko kile kitokanacho na furaha na shangwe huleta mabadiliko yanayoweza kupimwa katika mfumo wa kinga mwilini mwa mtu. Unaweza kabisa kuusaidia mwili wako kupigana na ugonjwa kwa vizuri zaidi ukiwa na furaha! Uchunguzi huo huonyesha jinsi akili na mwili vinavyofanya kazi yao kwa pamoja kwa ushirikiano wa karibu sana.

Katika maelfu ya miaka iliyopita Neno la Mungu lilidokeza kuwapo kwa uhusiano huo wenye nguvu kati ya akili na mwili ambao ni hivi karibuni tu umekubaliwa na kuingizwa katika nadharia ya kiganga:

Mithali 17:22
"Moyo uliochangamka ni dawa nzuri, bali roho iliyopondeka huikausha mifupa"

Kulingana na mtume Yohana, Je, Ni kwa karibu jinsi gani uhusiano huo uliopo kati ya akili na mwili unaathiri usitawi wetu wa kiroho?

3 Yohana 1:2
"Mpenzi wangu, nakutakia mafanikio mema ya kila aina; nakutakia afya njema ya mwili kama ulivyo nayo rohoni"

Muumbaji wetu anataka sisi tupate " kufurahia kuwa na afya njema " Neno la Mungu linaweza kutumika kama chemchem yetu ya afya, pamoja na kuwa chemchem yetu ya uzima wa milele.

Kwa kuwa usitawi wetu kimwili na kiakili na kiroho unakwenda bega kwa bega, Paulo anatoa kwetu ombi hili:

1 Wakorintho 10:31
"Mlapo mnywapo au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu"

Injili inajumuisha mambo yote mawili, uponyaji wa mwili na uponyaji wa roho. Mtindo wa maisha uletao afya unaweza kutusaidia sisi kuwa Wakristo wenye uchangamfu mwingi.

Hapa zipo kanuni nane za kufuata endapo wewe kweli unataka kuishi maisha yenye afya na yenye manufaa mengi zaidi.